- 78,506 viewsDuration: 1:27Kiwango cha ushiriki wa Waafrika katika vita vya Urusi huenda kikawa kikubwa zaidi kuliko ilivyodhaniwa awali. Kwa mujibu wa serikali ya Ukraine, takribani wapiganaji 3,000 wameajiriwa na Urusi kutoka barani Afrika, na zaidi ya 300 tayari wameuawa vitani. Ni serikali chache tu, zikiwemo Kenya na Ghana, ambazo zimepinga hadharani, zikieleza wasiwasi kuhusu uajiri huo na hatima ya raia wao. Sammy Awami wa BBC alipata nafasi ya kipekee kutembelea kituo cha wafungwa wa vita magharibi mwa Ukraine, ambako wanaume wa Kiafrika sasa wamekwama kati ya vita, siasa, na mustakabali usio na uhakika. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw