Spika wa bunge la taifa apokea maombi manne kuhusu kubanduliwa kwa makamishna wanne wa IEBC

  • | K24 Video
    7 views

    Spika wa bunge la taifa amepokea maombi manne yanasukumia kubanduliwa afisini kwa makamishna wanne wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini . Spika Moses Wetangula ameagiza kamati ya sheria kushugulikia maombi hayo na kuwasilisha ripoti yake bungeni katika siku 14 zijazo. Yakijiri hayo, kamati ya bunge ya maombi ya umma pia imejukumiwa kuangazia ombi la shirika la watumizi wa bidhaa linaloibua maswali kuhusu utumizi wa shilingi bilioni 55 na serikali iliyoondoka mamlakani bila idhini ya bunge