Taasisi ya huduma ya vijana kwa taifa, NYS yaanzishwa Busia

  • | Citizen TV
    321 views

    Ni afueni kwa wakazi wa eneo bunge la Teso Kaskazini kaunti ya Busia kufuatia kuanzishwa kwa ujenzi wa taasisi ya Huduma ya vijana kwa taifa (NYS). vijana wanatarajiwa kunufaika pakubwa kwa kupata ujuzi wa kuwawezesha kuajiriwa au kujiajiri. Kwa muda mrefu, vijana kutoka Teso Kaskazini ambao walikuwa na ari ya kujiunga na taasisi ya NYS walilazimika kusafiri zaidi ya kilomita 95 hadi katika eneo la Turbo lililoko katika kaunti jirani ya Uasin Gishu ambapo huduma hizo hupatikana.