Takriban watu 10,000 wadhaniwa wamepotea kufuatia mafuriko makubwa Libya

  • | VOA Swahili
    662 views
    Takriban watu 10,000 wanadhaniwa wamepotea kufuatia mafuriko makubwa nchini Libya, afisa mmoja kutoka Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Jumuiya za Mwezi Mwekundu (IFRC) alisema Jumanne (Septemba 12). Kiasi cha robo ya mji wa mashariki mwa Libya wa Derna ulisombwa na mafuriko baada ya mabwawa kupasuka kutokana na dhoruba, na miili zaidi ya 1,000 imeopolewa hadi hivi sasa, waziri katika serikali hiyo inayodhibiti upande wa mashariki alisema Jumanne. “Idadi ya vifo ni kubwa na inaweza kufikia maelfu,” Tamer Ramadan, mkuu wa ujumbe wa IFRC nchini Libya, aliwaambia waandishi wa habari huko Geneva kupitia mtandao wa mawasiliano ya video kutoka Tunisia. Shirikisho hilo la IFRC linaweza kwa siku za karibuni kuomba ufadhili wa dharura kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko hayo nchini Libya. Reuters/UNTV #mafuriko #libya #derna #dhoruba #mabwawa #miili #waziri #serikali #voa #voaswahili #dunianileo - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.