Skip to main content
Skip to main content

Tazama jinsi droni ya Ukraine ilivyopiga kwenye fukwe yenye watu wengi

  • | BBC Swahili
    6,900 views
    Duration: 25s
    Maafisa wa Urusi wanasema kuwa watu wasiopungua saba, wakiwemo watoto watatu, wamefariki dunia kutokana na shambulio la droni ya Ukraine kwenye ufukwe ulioko kusini-magharibi mwa Urusi. Bado haijafahamika ikiwa droni hiyo ilidunguliwa kabla ya kutua kwenye ufukwe huo. Imeripotiwa kuwa huenda ilikuwa ikilenga kambi ya wanamaji ya Urusi iliyoko takriban kilomita 40 kutoka eneo la tukio, lakini Ukraine haijatoa maoni yoyote kuhusu tukio hilo. Ufukwe wa Gelendzhik ni moja ya maeneo yanayopendwa na watalii wa ndani wa Urusi kwa ajili ya mapumziko. #bbcswahili #urusi #ukraine Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw