Timu mbalimbali za waokoaji zaendelea kuitoa miili kutoka katika kifusi Morocco

  • | VOA Swahili
    378 views
    Timu mbalimbali za waokoaji zimeendelea kuitoa miili kutoka katika kifusi baada ya tetemeko la ardhi lililokuwa na nguvu ya 6.8 nchini Morocco kuangusha majumba na kuua watu zaidi ya 2,000. Timu za uokoaji katika mji wa Ouirgane, kilomita 60 kutoka Marrakech, walichimba katika matofali na zege ya majumba Jumatatu. Morocco imepeleka gari za kuchukua wagonjwa, waokoaji na wanajeshi katika mkoa huo kusaidia na juhudi za huduma za dharura. Makundi ya misaada yamesema kuwa serikali haijaomba msaada lakini imekubali kupokea misaada michache kutoka nje ya nchi. - AP #morocco #earthquake #MoroccoEarthquake - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.