Skip to main content
Skip to main content

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi imeitetea rekodi yake katika vita dhidi ya ufisadi

  • | Citizen TV
    570 views
    Duration: 7:10
    Tume ya maadili na kupambana na ufisadi imeitetea rekodi yake katika vita dhidi ya ufisadi, ikiripoti kiwango cha asilimia 72 cha hukumu na kurejeshwa kwa shilingi bilioni 7.8 fedha za umma zilizoibwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Akizungumza katika kikao na wanahabari hapa jijini nairobi, afisa mkuu wa tume hiyo, abdi mohamud amesema kuwa utekelezaji wa sheria pekee hautoshi, na kuhimiza kuimarishwa kwa mikakati ya kuzuia ufisadi pamoja na matumizi ya mifumo ya kidijitali.