- 8,414 viewsDuration: 2:20Kupitia ucheshi wake wa kipekee, Gasper Kagonda maarufu kama @gasper_comic ameweza kuwafanya maelfu ya watu kucheka huku akigusa masuala yanayoihusu jamii. Lakini kadri maudhui yake yanavyozidi kugusa sekta nyeti na mijadala ya umma, ndivyo maswali yanavyoibuka kuhusu mipaka ya uhuru wa kujieleza na changamoto ambazo watayarishaji wa maudhui wanaweza kukutana nazo wanapochagua kutumia sanaa kuibua mijadala. Katika mahojiano na Mwandishi wa BBC @frankmavura, Gasper amezungumza kwa uwazi jinsi anavyoamua kile cha kuchapisha, namna anavyotumia mafumbo kama “Malawi” kuwasilisha ujumbe, na iwapo huwa anawaza kuhusu usalama wake binafsi au mustakabali wa kazi yake kabla ya kuchapisha maudhui yanayoweza kuzua mjadala. - - #bbcswahili #tanzania #siasa #foryou #vichekesho #nyotawaafrikamashariki Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw