Uchukuzi na Biashara zatatizika kwa muda Karatina, Nyeri

  • | Citizen TV
    8,617 views

    Shughuli za Uchukuzi na Biashara zilitatizika kwa muda mjini Karatina kaunti ya Nyeri, wafuasi wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na wale wa Mbunge wa Mathira Eric Wamumbi kukabiliana. Chanzo cha mgongano huu kikiwa maandamano yaliyokuwa yameandaliwa na wafuasi wa Gachagua kuikashifu serikali.