- 308 viewsUchunguzi wa maiti ya Bernard Omae aliyefariki akiwa ndani ya seli za polisi katika kituo cha polisi cha Kibera umebaini kuwa alifariki kutokana na majeraha mabaya mwilini. Familia yake ilidai kuwa maafisa wa polisi waliomkamata katika eneo la Utawala kwa madai ya wizi wa pikipiki walimpiga vibaya. Na kama anavyoarifu Franklin Wallah, uchunguzi wa mshukiwa mwingine aliyefariki katika kituo cha polisi cha Kariobangi North pia umethibitisha kuwa alikufa kutokana na kupigwa na kifaa butu kichwani.