Uchunguzi kuhusu kisa cha moto katika Shule ya Wasichana ya Utumishi umebaini kuwa wanafunzi saba wanaodaiwa kuhusika na kuanzisha moto huo walikuwa wakigoma kufuatia hatua ya shule kubadilisha tarehe za mitihani.
Inadaiwa pia walipinga kulazimishwa kugharamia hafla ya kitamaduni pamoja na madai ya kutoruhusiwa kwenda nyumbani baada ya shule jirani kugoma.
Wanafunzi hao saba, ambao bado wanazuiliwa, wamewaeleza maafisa wa upelelezi kuwa nia yao haikuwa kuwasababishia madhara wenzao, bali walichoma bweni kama njia ya kuonyesha ghadhabu yao.
Uchunguzi zaidi unaendelea kubaini mazingira kamili ya tukio hilo.