- 314 viewsDuration: 1:19Muungano wa walimu KUPPET umetaja uhaba wa walimu wa masomo ya stem katika gredi ya kumi kama changamoto kuu shuleni na kuitaka serikali kuajiri walimu wenye uzoefu wa masomo hayo. Wakiongozwa na katibu wa kuppet tawi la mombasa lynette kamadi amedai hadi sasa shule nyingi pwani bado hazijaanza masomo hayo kutokana na uhaba wa vifaa na walimu katika masomo hayo. Kuppet wameunga mkono hatua ya bunge kuishinikiza mageuzi katika wizara hiyo.