Ukulima wa Mwani umevutia wakulima wengi Kwale

  • | Citizen TV
    185 views

    Watafiti na wakulima wa mwani katika kaunti ya Kwale wamependekeza mmea huo kuorodheshwa kama zao la kibiashara kutokana na faida zake. Ukulima wa mwani umevutia wakulima wengi na kuimarisha uchumi wa Bahari kulingana na utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti wa uvuvi na bahari (KEMFRI) ambapo sasa mumea huo Unatumika kutengeneza mafuta, sabuni na hata vyakula. Zaidi ya wakulima 800 wamehusishwa kwenye kilimo hicho.