- 4,122 viewsDuration: 1:41Zanzibar, idadi ya vijana wanaojiandaa kupiga kura kwa mara ya kwanza inaongezeka. Miongoni mwao ni Saimah Said Hamad @lovely_say01 mwanafunzi wa saikolojia aliyejiunga na Pamoja Youth Institute, kundi linalotoa elimu kuhusu umuhimu wa kushiriki kwenye uchaguzi. Saimah anasema kushiriki katika uchaguzi wa 2025 ni fursa ya kusikika na kuchangia mustakabali wa jamii yake. Bara, wapiga kura wa mara ya kwanza pia wameonyesha hamasa, wakiiomba serikali kuongeza elimu kwa wananchi kuhusu mchakato na umuhimu wa kupiga kura. Mwandishi wa BBC @elizabethkazibure na maelezo zaidi. 🎥: @frankmavura - - #bbcswahili #vijana #uchaguzi2025 #zanzibar