- 3,487 viewsDuration: 3:05Viongozi wa Upinzani wameisuta serikali kwa kufumba macho wakati ambapo uhuni unaendelea kukithiri katika baadhi ya maeneo nchini. Wakirejelea kisa cha hivi maajuzi ambapo seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi alivamiwa na kujeruhiwa huko Kisumu, viongozi hao ambao walizuru Kaunti ya Machakos wamesisitiza kuwa ni Sharti Katibu Wa usalama wa kitaifa Raymond Omollo Kuchukuliwa Hatua na uchunguzi kufanywa kuhusu matukio hayo ya uhuni.