- 803 viewsDuration: 2:18Viongozi wa Upinzani wamepongeza hatua ya wapiga kura kusimama kidete katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou Alhamisi licha ya vurumai iliyoshuhudiwa kati ya wakazi na wahuni wanaodaiwa kupanga kuvurugu kwenye uchaguzi huo. Viongozi hao wakisema upinzani umejipanga vilivyo kuhakikisha kura za 2027 zinalindwa zaidi ya yaliyoshuhudiwa Ol Kalou. Viongozi hao akiwemo Naibu Kinara wa Jubilee Fred Matiangi, Kiongozi wa PLP Martha Karua na wenzao wa Linda Mwananchi waliokuwa wakizumgumza katika maeneo tofauti wameelezea matumaini yao ya kutwaa uongozi wa Taifa katika uchaguzi mkuu mwakani.