- 355 viewsDuration: 3:07Wizara ya Elimu imesema upungufu wa fedha katika bajeti na ucheleweshaji wa fedha kutoka Hazina ya Taifa ndio chanzo kikuu cha changamoto za kifedha zinazokabili shule, vyuo vya TVET na vyuo vikuu. Akilihutubia Bunge, Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba amesema kuna upungufu wa takriban shilingi bilioni 29 unaohitajika kufadhili vyuo vikuu. Amesema wizara inaendelea kutafuta vyanzo mbadala vya mapato huku ikishinikiza kuongezwa kwa mgao wa fedha kwa sekta ya elimu.