'Urafiki wetu haujasambaratika': Wasanii wawili kutoka Israel-Gaza

  • | BBC Swahili
    584 views
    Miaka miwili iliyopita, mtindo wa kushindana kuimba nyimbo za kufoka foka kwa Kiebrania na Kiarabu cha Palestina ulisambaa sana mtandaoni. Uriya Rosenman ni mwalimu wa Kiyahudi kutoka Israeli na Sameh Zakout ni mwimbaji na mwigizaji wa Palestina. Mradi wao wa DUGRI hutumia muziki kupigania kuishi kwa ushirikiano. Marafiki wa Uriya waliuawa na kutekwa nyara tarehe 7 Oktoba. Na kufuatia mashambulizi ya Gaza Sameh alipoteza baadhi ya wanafamilia. Licha ya majonzi hayo, wanaendelea kuamini kuwa kunapaswa kuwa na njia nyingine ya kutafuta suluhu na bila kutumia nguvu #bbcswahili #gaza #hamas Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw