- 251 viewsDuration: 1:16Tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka imesema iko tayari kwa uchaguzi mdogo utakaofanyika maeneo tofauti nchini siku ya Alhamisi. Akizungumza baada ya kikao na maafisa wa usalama huko Siakago Kaunti ya Embu, afisa mkuu wa IEBC Marjan Hussein Marjan amesema kwamba makarani wote wako tayari na kwamba vifaa vya kupigia kura vitasafirishwa katika vituo vyote vya kupigia kura hapo kesho.