Muungano wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake umetoa wito wa kushirikishwa kwa watu walio na ulemavu katika uundaji wa sera na miongozo, ili kuimarisha juhudi za pamoja za kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wenye ulemavu. Haya yanajiri kufuatia utafiti wa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake mwaka 2019, ambao uliashiria kuwa asilimia 73.1 ya wanawake wenye ulemavu wamewahi kukumbana na aina moja au nyingine ya ukatili wa kijinsia.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive