- 1,364 viewsDuration: 3:30Utata wa umiliki wa ardhi ya zaidi ya ekari 200 katika kaunti ya Kiambu inayodaiwa kuwahusisha watu mashuhuri serikalini, sasa umeelekea mahakamani. Hii ni baada ya wakurugenzi wa kampuni ya Ndunde Investments kuwasilisha kesi wakitaka waliovamia ardhi kuzuiwa kuingia eneo hilo na kutouza au kubatilisha vyeti vya umiliki. Wakurugenzi hao wanasema wamekuwa wamiliki wa ardhi hiyo kwa miaka 26 na kwamba wale wanaotaka kuichukua wanatumia stakabadhi ghushi.