Skip to main content
Skip to main content

Utendakazi hospitalini Mama Lucy

  • | Citizen TV
    461 views
    Duration: 1:38
    Hospitali ya Mama Lucy Kibaki imeanzisha mpango kamili wa usajili wa papo kwa papo wa Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) kwa wagonjwa wote ili kuhakikisha hakuna anayekosa matibabu kwa sababu ya kukosa fedha. Kila anayefika hospitalini sasa anaongozwa kujisajili katika mfumo wa SHA kabla au wakati wa kupata huduma, hatua inayoiwezesha hospitali kutoa matibabu kwanza na kufuatilia malipo baadaye kupitia SHA. Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Frederick Obwanda, alisema kituo hicho hupokea zaidi ya wagonjwa 1,500 kila siku na kwamba usajili wa wote katika SHA umeondoa ucheleweshaji wa huduma uliokuwa unasababishwa na madeni ya matibabu.