- 325 viewsDuration: 1:57Zaidi ya vijana 25 mjini Malindi wamenufaika na msaada wa Boti tatu zenye thamani ya shilingi milioni 15 kutoka Kwa shirika la Almdaad ili kuimarisha uchumi wa baharini. Wakizungumza kwenye hafla hiyo wavuvi hao wamesema boti hizo zitaimarisha shughuli zao za uvuvi pamoja na kuokoa maisha ya wale wanaobebwa na mawimbi makali. Mkurugenzi wa kitaifa wa wakfu wa Almdaad Abdulrahman Abdala amesema hatua hiyo inalenga kusaidia wavuvi kujikimu kimaisha. Aidha afisa mkuu wa biashara na uvuvi kaunti ya Kilifi Zamzam Mohamed amesema serikali ya kaunti inashirikiana na wawekezaji zaidi ili kuimarisha uchumi wa baharini.