Skip to main content
Skip to main content

Vijana kaunti ya Busia wahimizwa kujisajili kwa wingi kama wapigakura

  • | Citizen TV
    359 views
    Duration: 2:13
    Vijana katika kaunti ya Busia wamehimizwa kutumia fursa hii na kujitokeza kwa wingi kuhakiki upiga kura wao ili kuhakikisha ushiriki wao katika uchaguzi ujao, mbali na kuhamasisha usajili wa wapiga kura... Vijana hao wa kaunti ya mpakani wametakiwa kushiriki zoezi linaloendelea la uhakiki na wito wa niko kadi unaosukumwa na vijana wa kizazi cha Gen Z unaolenga kuwahimiza vijana kujisajili kote nchini, wakipinga vurugu wakati wa kampeini na uchaguzi. Wanachama wa chama cha UDA katika kaunti ya Busia wamesema kuwa tayari wameweka mikakati kabambe ambayo itafanikisha zoezi hilo hata nyanjani licha ya changamoto za mtandao. Wakati huo huo, wanachama hao wameunga mkono uamuzi wa katibu wa kitaifa wa chama hicho Hasan Omar, wa kupinga tangazo la kutaka kugawana maeneo ya kisiasa (party zoning) wa nyadhifa mbali mbali za kisiasa kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao wa 2027.