- 169 viewsDuration: 1:55Muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu kaunti ya Taita Taveta umesema kwamba unaendelea na zoezi la kujiandikisha kuwa wapiga kura tayari kwa uchaguzi mkuu ujao wa 2027. Wakiongozwa na rais wa wanafunzi kaunti hiyo Liz Wakesho wanafunzi hao wanasema zoezi la usajili wa wapigakura linaloendelea linatoa nafasi mwafaka kwa wanafunzi kushiriki uchaguzi huo mkuu. Haya yanajiri huku wito ukitolewa kwa wanafunzi hao kujiunga na vyama vya kisiasa ili kushinikiza mageuzi yao ndani vya vyama hivyo.