VIJANA WADOGO WAANZISHA KAMPENI YA MAZINGIRA KUPITIA KANDANDA MALINDI

  • | KNA Video
    12 views
    Vijana wadogo wenye umri kati ya miaka 9-13 wameanzisha kampeni ya kutumia kandanda kuwaleta pamoja vijana wenzao ili kuboresha mazingira eneo la Malindi kaunti ya kilifi. Kulingana na Jada Neema, mwanamazingira eneo hilo, hatua ya kutumia kandanda inatoa mvutio mkubwa miongoni mwa wanarika anaosema huchangia pakubwa kulinda mazingira. Wakati huo huo Ruth Anyango, mwanamazingira eneo hilo anasema kwasasa juhudi zao kutumia vijana kwa njia ya michezo zinaonekana kuzaa matunda. Aidha mkufunzi wa vijana hao Rashid Shedu ameunga mkono mfumo huo akisema unatoa nafasi Kwa vijana kuonesha talanta zao wakati wanapo tunza mazingira.