Vikao vya umma dhidi ya hatma ya Gachagua kuandaliwa kaunti zote 47 nchini

  • | Citizen TV
    5,096 views

    Kuanzia hapo kesho Wabunge wanatarajiwa kurejea katika maeneo bunge yao kuandaa shughuli ya kuchukua maoni kutoka kwa wakenya kabla ya vikao vya kujadili hoja ya kumtimua naibu rais rigathi gachagua. Vikao hivi vikitarajiwa kufanyika kabla ya siku ya jumanne, ambapo Gachagua atakuwa na muda wa saa mbili unusu kujitetea mbele ya wabunge.