Viongozi wa Azimio waitaka serikali iangazie mahangaiko ya wakenya

  • | K24 Video
    217 views

    Viongozi wa muungano wa Azimio wamekashifu vikali tume ya kupambana na ufisadi kwa kile wanachodai ni vitisho kutoka kwa serikali ambayo inatumia kesi za ufisadi kuzima upinzani. Viongozi hao wanashikilia kuwa hawatatishwa katika majukumu yao na kuwa watazidi kutetea wakenya. Haya yanajiri siku chache tu baada ya afisi ya mkurungezi wa mashtaka ya umma, ODPP, kuamuru aliyekuwa gavana wa murang’a mwangi wa iria na wengine saba kufunguliwa mashtaka baada ya kukiuka sheria ya ununuzi kati ya mwaka wa 2014 na 2016 alipokuwa gavana.