Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa jamii za Luo na Kalenjin warai jamii zote mbili zishirikiane 2027

  • | Citizen TV
    745 views
    Duration: 1:44
    Viongozi kutoka jamii za Luo na Kalenjin wametoa wito kwa wakenya kujisajili au kuhakikisha usahihi wa majina Yao katika sajili ya wapigakura, ili kushiriki vilivyo katika uchaguzi mkuu ujao. Baraza la wazee wa jamii hizo mbili walikongamana kaunti ya Siaya, katika maombi maalum nyumbani kwa katibu katika wizara ya Afya, Ouma Oluga. Aidha, viongozi hao walirai jamii zote mbili kuungana na kususia semi za uchochezi zilizoenea siku za hivi punde, ambapo Cheche za siasa zinaonekana kushika kasi. Viongozi hao pia walielezea umuhimu wa utangamano ili kuiwezesha serikali kutekeleza miradi ya maendeleo mashinani