Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa Jubilee wakemea rabsha za siasa

  • | Citizen TV
    971 views
    Duration: 3:29
    Baadhi ya viongozi wa chama cha Jubilee wameshutumu vikali visa vya uvamizi wa mikutano ya upinzani, wakiisuta idara ya polisi kwa kushirikiana na wahuni kuvuruga mikutano hiyo. Wakizungumza kwenye uzinduzi wa ofisi ya chama cha Jubilee mjini Nyamira, viongozi hao wakiongozwa naye katibu mkuu wa chama hicho Moitalel Ole Kenta wamesema mikutano yao ni ya amani na kuiomba idara ya polisi kutotumika kisiasa. Aidha viongozi hao wameisuta serikali yake rais William Ruto, kwa madai ya kufeli kutekeleza ahadi walizotoa kwa wakenya wakati wa kampeni.