Viongozi wa Kanisa Katoliki wameitaka serikali kuwajibika

  • | Citizen TV
    519 views

    Viongozi wa Kanisa Katoliki wameitaka serikali kujinasua kutoka kwenye maruweruwe ya kampeni na kuanza kuchapa kazi ili kuwatimizia wakenya ahadi walizotoa. Aidha viongozi hao wameitaka serikali kuongeza juhudi za kuhakikisha wakenya milioni nne wanaokabiliwa na njaa na mifugo wanaongamia kwa kukosa lishe wamefikiwa na msaada. Na kama anavyoarifu Francis Mtalaki, viongozi hao wanaitaka serikali kuondoa mapendekezo ya kuongeza ushuru kwa sasa.