Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa kanisa wataka serikali kudumisha amani Angata Barrakoi

  • | Citizen TV
    210 views
    Duration: 2:45
    Uongozi wa kanisa la kiadventista tawi la west Kenya wameomba idara ya Usalama kuingilia kati na kutatua mzozo ambayo imekuwa imekita mizizi katika eneo la Angata Barrakoi katika mpaka wa kaunti ya Migori na Narok..... Uongozi wa kanisa Hilo wanasema wameghadhabishwa na Hali tete katika eneo Hilo ambayo imeleta madhara mengi kwa wakaazi. Wakizungumza katika eneo la Gwitembe baada ya zaidi ya familia 300 kupoteza makazi Yao katika ushambulizi wa hivi majuzi, rais wa kanisa la kiadventista tawi la west Kenya, Samuel Misiani alieleza kuwa ni wakati mwafaka wa Serikali kupitia idara ya Usalama kujitokeza kimasomaso kutatua mzozo wa ardhi baina ya wenyeji wa kipsigis na wakuria wanaoishi katika Maeneo hayo.....