- 2,640 viewsDuration: 2:02Baadhi ya viongozi serikalini wanaendelea kumsuta aliyekua rais humu nchini uhuru Kenyatta kwa madai ya kueneza siasa za ukabila. Wakizungumza katika eneo la Dabaso Kilifi Kaskazini walipokua wakihiuhuria mazishi ya mamake mbunge wa eneo hilo owen baya, viongozi hao wamesema kuwa matamshi ya kenyatta yanachangia kuwagawanya wakenya kwa misingi wa ukabila. Magavana wa Kilifi Gideon Mung’aro na mwenzake wa Mombasa Abdulsamad sharif wamedokeza kuwa siasa ya ukabila haina Nafasi humu nchini, wamewataka viongozi badala kujipigia debe kupitia utekelezaji wa miradi inayolenga kuboresha maisha ya wakazi.