Viongozi wa kenya kwanza wawasuta wapinzani

  • | Citizen TV
    702 views

    Viongozi wa serikali wamewasuta wapinzani kwa kuendeleza siasa za mgawanyiko na kuwataka kuuza ajenda zao badala ya kuwachochea wananchi. Wakiongozwa na naibu rais Profesa Kithure Kindiki, viongozi hao wamewarai wananchi kumpa rais nafasi ya kuwatimizia ahadi alizotoa. Aidha wametetea msururu wa michango ya kuwapiga jeki wafanyibiashara wakisema unalenga kuinua uchumi wa makundi mbalimbali.