- 3,471 viewsDuration: 3:18Viongozi wa kidini wamekana kuwa waliwapotosha Wakenya kwenye uchaguzi uliopita. Askofu wa Kanisa la Katoliki Jimbo la Mombasa Martin Kivuva amemkosoa rais mstaafu Uhuru Kenyatta akisema kuwa ufisadi na hongo kwa wapiga kura ndio donda sugu linalochangia kwa uongozi mbaya nchini. Viongozi wa kidini pia wametaka cheche za matusi kukoma wakitoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha kama wapiga kura.