Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa kisiasa waonywa dhidi ya vurugu mikutanoni na waziri wa usalama wa kitaifa Murkomen

  • | Citizen TV
    284 views
    Duration: 1:55
    Waziri wa Usalama wa kitaifa, Kipchumba Murkomen, ametoa onyo kali kwa wanasiasa wanaowatumia vijana kuzua vurugu katika mikutano ya kisiasa nchini, akisema serikali haitavumilia hulka hiyo ambayo inatishia usalama wa taifa. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Cherangany Unity Cup, yanayolenga kuimarisha mshikamano wa jamii zinazoishi katika mpaka wa kaunti za Trans Nzoia na Elgeyo Marakwet, Murkomen amedokeza kuwa kuna haja ya kuwahusisha vijana katika shughuli za maendeleo na miradi inayowaongezea kipato, badala ya kuwatumia katika siasa...