Viongozi wa Kisii watakiwa kushirikiana zaidi kwa maendeleo

  • | Citizen TV
    583 views

    Spika wa Bunge la Kitaifa amehimiza viongozi waliochaguliwa nchini kuweka tofauti zao za kisiasa kando na kuwafanyia kazi wananchi. Akizungumza eneo la Kisii alipohudhuria hafla ya kuchangisha fedha katika kanisa la katoliki la Nyabiosi eneobunge la Bonchari, Wetangula alitumia fursa hiyo kuongoza mapatano kati ya Gavana wa Kisii Simba Arati na Seneta wa kaunti hiyo Richard Onyonka ambao wamekuwa wakikwaruzana kisiasa tangu kuchaguliwa kwao