- 1,636 viewsDuration: 2:30Mjadala kuhusu wadhifa wa naibu Rais katika uchaguzi mkuu ujao unaendelea kuibuka, huku baadhi ya viongozi wa Mlima Kenya wakisisitiza nafasi hiyo inapasa kusalia katika eneo hilo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Viongozi hao walikuwa wakizungumza huko Nyeri katika kikao cha kuzungumza na wananchi ambacho pia kilihudhuriwa na maafisa wa serikali waliopigia debe serikali.