Viongozi wa serikali wameendelea kuishutumu upinzani kwa kupinga juhudi za serikali za kujenga vituo vya karantini nchini, wakisema hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya kujiandaa endapo kutatokea mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Wakizungumza katika hafla tofauti mjini Eldoret na Kaunti ya Busia, viongozi hao walisema vituo hivyo ni muhimu katika kuimarisha utayari wa taifa kukabiliana na dharura za afya ya umma.
Aidha, waliwataka wananchi kuunga mkono mipango ya serikali na kuepuka kuruhusu wanasiasa kueneza chuki au kuwagawanya kwa misingi ya kisiasa.
Viongozi hao walisisitiza kuwa masuala ya afya ya umma yanapaswa kushughulikiwa kwa umoja na bila siasa.