- 5,436 viewsDuration: 2:42Vyombo viwili vya anga vya Voyager 1 na Voyager 2 vilitengenezwa na kutumwa angani vikitarajiwa kufanya kazi kwa miaka mitano tu. Hata hivyo, karibu miaka 50 baadaye bado vinaendelea kufanya kazi na kusafiri mbali zaidi na Dunia kuliko kitu chochote kingine kilichotengenezwa na binadamu. Mwanasayansi wa mradi, Linda Spilker, anazungumzia jinsi vyombo hivyo vilivyobadilisha uelewa wetu kuhusu mfumo wa jua kwa kutuma taarifa na picha muhimu kutoka sayari mbalimbali. Na wazo kwamba viumbe wa nje ya dunia wanaoweza kuwepo huenda wakavipata siku moja na hata kurudi kututembelea hapa Duniani. - - #bbcswahili #NASA #sayansi #teknolojia Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw