Vyama vya kisiasa vimewasilisha majina ya wanaopendekezwa kuwa wabunge wa EALA

  • | Citizen TV
    627 views

    Vyama vya kisiasa vimewasilisha majina ya watu wanaopendekezwa kuwa waakilishi katika bunge la Afrika mashariki. Muungano wa Kenya Kwanza ambao umepewa nafasi tano, umewasilisha majina 15 huku muungano wa azimio ukiidhinisha majina 11. Majina hayo yamewasilishwa bungeni. Miongoni mwa walioteuliwa ni bintiye kinara wa Azimio Winnie Odinga, mwanawe kinara wa Wiper Kennedy Musyoka, kiongozi wa vijana wa UDA mkoa wa Nyanza Joel Okengo na Anne Too. Wabunge sasa watapiga kura alhamisi ijayo kuwachagua tisa bora watakaoelekea bungeni Arusha, Tanzania.