Mamia ya waandamanaji wamejitokeza katikati ya jiji la Nairobi wakilalamikia kile wanachokitaja kuwa utepevu wa polisi na serikali katika kukabiliana na visa vya mauaji ya wanawake, pamoja na matukio ya kutoweka na kuuawa kwa watoto.
Waandamanaji hao wametaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kuimarisha usalama na kulinda makundi yaliyo hatarini zaidi katika jamii.
Wamesisitiza kuwa hali hiyo imekuwa ikiripotiwa mara kwa mara bila hatua madhubuti kuchukuliwa, jambo linaloongeza hofu miongoni mwa wananchi.
Kama anavyoripoti Franklin Wallah, serikali sasa imetakiwa kuweka mikakati kabambe ya kukabiliana na ongezeko la visa hivyo.