Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu kutoka kaunti ya Garissa, wamelalamikia ukosefu wa mkalimani katika vituo vya polisi, wakisema inakuwa vigumu kutafsiri taarifa za waathiriwa wa dhulma vya kijinsia, haswa kwa walemavu.
Kwenye mkutano wa kutathmini changamoto zinazoibuka, wanaharakati hao wamesema hali hiyo inachangia waathiriwa kukosa haki na kuchangia ongezeko la unyanyapaa miongoni mwao.Aidha wanataka ushirikiano baina ya wadau wote kwenye mfumo wa haki, kuhakikisha kesi zinazohusu dhulma za kijinsia zinakamilika kwa muda mfupi.