Wabunge kutoka Garissa wapinga mpango wa serikali wa kujumuisha wakimbizi na jamii za karibu

  • | Citizen TV
    543 views

    Wabunge kutoka kaunti ya Garissa wamepinga vikali mpango wa serikali na shirika la Umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi -UNHCR - kutaka kujumuisha wakimbizi na jamii zinazoishi karibu na kambi za wakimbizi. Wabunge hao wakiongozwa na mbunge wa Daadab Farah Maalim wamekashifu serikali na UNHCR kwa kuendeleza mpamgo huo bila kuhusisha jamii zinazoishi karibu na kambi hizo. Wabunge hao pia wamemkashifu katibu katika wizara ya uhamiaji Julius Bitok kwa ubaguzi kuhusiana na uteuzi wa maafisa wanaosimamia maswala ya wakimbizi