- 171 viewsDuration: 1:55Viongozi kutoka kaunti ya Tana River wamelaumu ada za masomo ya ziada zinazotozwa na walimu kama chanzo cha matokeo mabaya ya mitihani ya kitaifa katika eneo hilo. Kwenye mkutano ya siku ya elimu kaunti hiyo, viongozi hao wamesema wanafunzi wanasalia nyumbani kwa muda mrefu kutokana ada hizo ilhali karo yote imelipwa na wazazi. Viongozi hao waliafikia kufanya elimu ya shule ya msingi na sekondari kuwa bure pindi ripoti ya idadi ya wanafunzi katika maeneo bunge yote tatu itakapotolewa.