Wabunge watakiwa kuratibu sheria kukabili mauaji ya wanawake

  • | KBC Video
    18 views

    Zaidi ya asilimia 60 ya visa vya mauaji ya wanawake nchini hutokea nyumbani, aghalabu kufuatia kipindi kirefu cha dhuluma zisizoripotiwa. Haya yaliwekwa wazi na Dkt. Nancy Baraza aliye mwenyekiti wa jopokazi lililoteuliwa na Rais William Ruto kuchunguza dhuluma za kijinsia pamoja na mauaji ya wanawake humu nchini, wakati wa mkutano wa kundi la kitaifa la sekta ya jinsia jijini Nairobi. Dkt. Baraza alitoa wito kwa wabunge kupitisha sheria itakayoorodhesha mauaji ya wanawake kama uhalifu tofauti na mauaji mengine.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive