Wafanyabiashara walioathiriwa na maandamano waanzisha kampeni za michango

  • | Citizen TV
    2,635 views

    Wafanyabiashara waliopoteza mali yao katika maandamano ya wiki jana wanahangaika kujenga upya maisha na biashara zao. Wengi walipata hasara kubwa baada ya wahuni kutumia maandamano hayo kupora maduka. Bidhaa za thamani ya mamilioni ya pesa ziliharibiwa katika machafuko hayo. Katika juhudi za kujikwamua, baadhi ya wafanyabiashara wameanza harakati za kuchangisha fedha, wakitumia mitandao ya kijamii kuomba msaada kutoka kwa marafiki, wahisani, na wakenya wenzao. Walizungumza na mwanahabari wetu Ben Kirui na hii hapa taarifa hiyo.