Wafanyakazi zaidi ya 2,000 walighushi vyeti vya masomo kutokana na ripoti ya PSC

  • | Citizen TV
    761 views

    Tume ya kuajiri wafanyikazi wa Umma nchini (PSC) imesema kwamba zaidi ya wafanyikazi 2,000 wa umma wametumia stakabadhi ghushi za elimu ili kupata ajira. Akiwasilisha ripoti maalum ya Uchunguzi huo Kwa Tume ya EACC na idara ya DCI, mwenyekiti wa tume hiyo balozi Anthony Muchiri amesema kwamba wizara ya Usalama na hospitali ya rufaa ya Kenyatta ni miongoni mwa taasisi zinazongoza kwa wingi wa wafanyakazi wenye vyeti bandia.