Wafanyibiashara Bill na Melinda Gates kuzuru kaunti ya Makueni

  • | Citizen TV
    941 views

    Mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill Gates na aliyekuwa mkewe Melinda Gates wanazuru kaunti ya Makueni kutathmini huduma za afya zinavyotolewa kaunti hiyo. Wawili hao wanazuru hospitali ya Mother and Child inayoshughulikia kina mama na watoto, kabla ya kukutana na maafisa wa idara ya afya katika hospitali ya Kathonzweni. Kwenye ziara hiyo ambayo itahudhuriwa na gavana Mutula kilonzo jnr, Gates pia atazuru mashamba ya wakulima wawili walioweka mikakati ya kudhibiti mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha mimea yao imenawiri. Michael Mutinda anahudhuria hafla hiyo na anaungana nasi mubashara kutoka makueni