Wafanyibiashara Nyamira walalamikia hasara kufuatia maandamano ya Azimio

  • | Citizen TV
    501 views

    Wafanyibiashara mjini Nyamira wamelalamikia hasara, kufuatia maandamano ya Azimio. Wakizungumza na wanahabari mjini Nyamira, wafanyibiashara hao wamesema walilazimika kufunga maduka yao kwa kuhofia uporaji. Wafanyibiashara hao wanamwomba Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kutafuta mwafaka na kusitisha maandamano ama kuhakikisha maandamano hayo yanafanyika kwa amani bila kutatiza shughuli za kibiashara.